Sayari za mfumo wa jua

Uliza UjibiweAina: SayansiSayari za mfumo wa jua
Muchai aliuliza Mwaka 1 zilizopita

Ningependa kujua sayari zote kwa Kiswahili kama zinavyoandamana.

Majibu 2
Jibu Bora
Kipala alijibu Miezi 9 zilizopita

Samahani lakini orodha hapo juu si sahihi. Majina ya sayari 6 za kwanza kutoka Jua yalijulikana kwa Kiswahili tangu muda mrefu ni kama yafuatayo:

 1. Utaridi (Mercury)
 2. Zuhura au Ng’andu (Venus)
 3. Dunia (Earth)
 4. Mirihi (Mars)
 5. Mshtarii (Jupiter)
 6. Zohali (Saturn)

Kwa jumla majina haya yalipokelewa kutoka lugha ya Kiarabu ambayo zamani ilikuwa lugha kuu ya elimu hasa kuhusu nyota. Isipokuwa kwa sayari ya pili kuna pia jina asilia la Kibantu yaani Ng’andu kwa sababu hii ni sayari inayongaa kushinda nyota zote.
Sayari zinazofuata hazikujulikana kwa watu wa kale kwa sababu hazionekani kwa macho matupu. Wala Wasahili wala Waarabu hawakuzijua. Zilianza kugunduliwa tangu kupatikana kwa darubini, miaka 400 iliyopita. Majina yao ni
7. Uranus
8. Neptun
Hakuna sayari ya tisa tena inayojulikana; vitabu vingi vinataja hapa Pluto iliyogunduliwa mwaka 1930. Lakini baada ya kukuta vitu vingine vilivyofanana na Pluto wataalamu walijalidiana kama hizi zote ni sayari pia au ni kitu gani inayostahili kuitwa vile? Hapo Umoja wa Kimataifa ya Astronomia uliamua mwaka 2006 kutohesabu Pluto tena kati ya sayari kamili. Inaitwa sasa “sayari kibete” (dwarf planet) pamoja na Ceres , Haumea, na Eris.
Habari nyingi zaidi kuhusu maswali haya unapata hapa katika makala ya “mfumo wa jua” kwenye wikipedia ya Kiswahili (sw.wikipedia.org)

Mwanagenzi Msimamizi alijibu Miezi 7 zilizopita

Shukran kwa jibu lako na ufafanuzi mwafaka.

Judith Momanyi alijibu Mwaka 1 zilizopita
 1. Zaibaki/zebaki – Sayari ya kwanza iliyo karibu sana na juu katika mpangilio wa umbali wa sayari kutoka kwa jua.
 2. Ngandu/zuhura – Sayari katika mfumeo wa jua ambaye ni ya pili kutoka kwenye jua.
 3. Dunia – Ni sayari ambayo watu, wanyama na mimea  huishi.
 4. Mirihi/sayari nyekundu – Sayari
 5. Mshtarii
 6. Zohali – sayari moja inayozunguka jua yenye peteo na miezi kumi na ni ya sita katika mpagilio wa umbali wa sayari kutoka kwa jua.
 7. Kausi
 8. Sarateni
 9. Utaridi
Jibu Lako